Hans Bonge Music

kwa ajili ya music ungana nami hapa http://www.hulkshare.com/hansbonge

Monday 7 October 2013

KUMBE ATA MASTAR WAKIKE WANAWE2MIA VIWEMBE

NCHINI Nigeria wiki iliyopita kulikuwa na gumzo la msichana aliyechanwa na  viwembe na rafiki yake akaharibika mno sehemu ya paji la uso kisa walikuwa wakigombea mwanaume. Wakati wengine wakihaha na tindikali upande wa pili wa ishu za kimapenzi, viwembe na kupigana chupa ndizo silaha za mahangamizi.

Katika ulimwengu wa mastaa kila kukicha matukio yanatokea mapya yakiwemo ya kufurahisha, kuhuzunisha na kushangaza.

Kwa upande wa mastaa wa kike Bongo, wamekuwa na vituko vingi ikiwa ni pamoja na wao wenyewe kwa wenyewe kupigana na kuchanana viwembe kisa mapenzi. Ishu kubwa hapa ni kugombea wanaume kunakosababisha yote hayo.

Hivi karibuni kumezuka wimbi la mastaa kupigana wenyewe kwa wenyewe au kupigwa na warembo wengine wa mjini na silaha kubwa inayotumika ni viwembe na chupa kisa kikubwa kikiwa ni wivu au kusalitiana katika mapenzi kwani utakuta msanii anakuwa na uhusiano na mwanaume ambaye anajua ni wa rafiki yake na alishatambulishwa kuwa ni shemeji yake.

Watafiti wa mambo wanasema mastaa hawa wameamua kugeuza viwembe na chupa kuwa silaha zao za maangamizi kutokana na kukosa nguvu za kuhimili kipigo na mara nyingi mhusika anayetumia silaha hizi huwa anamlenga adui yake kwenye uso ili amuharibu sura na muonekano wake uwe mbaya ashindwe kuchukua waume za watu.

Leo tunakuletea listi ya baadhi ya mastaa wa Kibongo ambao wamewahi kuchanwa viwembe au chupa wenyewe kwa wenyewe au staa na wasichana wa mjini.




 Elizabeth Michael 'Lulu'.

ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’ Vs YVONNE MAXMILIAN
Lulu ni msanii wa filamu za Kibongo. Aliwahi kuchanwa na viwembe pembeni mwa paji la uso na mwanadada wa mjini anayejulikana kwa jina la Yvonne Maximilian na sababu kubwa ilikuwa ni ishu za kimapenzi.

AUNT EZEKIEL Vs YVONNE
Mwanadada huyu anayekimbiza katika kiwanda cha filamu Bongo hivi karibuni alichanwa na chupa mkononi na Yvonne ambaye ndiye alimchana Lulu pia na kumsababishia maumivu makali.

Aunt alijeruhiwa na kwenda kushonwa nyuzi kadhaa mkononi na sababu kubwa ilidaiwa ni mwanaume wa Yvonne anayejulikana kwa jina moja la Geofrey. Ilielezwa kuwa mwanaume huyo aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Aunt wakaachana. 

Yvonne alikuwa akimtuhumu Aunt kuwa anaendeleza uhusiano na mwanaume huyo, jambo ambalo lilimsababisha yeye kuchukua hatua ya kumchana chupa mkononi.

Kama siyo kujikinga kwa mkono, mwanamke huyo alitaka kumchana Aunt usoni katika Ukumbi wa Bilicanas jijini Dar ili kumharibu sura.
 
WATOTO WA MBWA Vs HAMISA

Wasanii watatu, Tiko Hassan, Mary Mawigi na Thecla wanaounda kundi moja linalojulikana kwa jina la Watoto wa Mbwa, miezi kadhaa iliyopita walidaiwa kumvamia msanii mwenzao aliyetajwa kwa jina moja la Hamisa nyumbani kwao maeneo ya Ilala na kumjeruhi usoni na kitu kilichodaiwa ni wembe.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wasanii hao walimvamia mwenzao huyo na kumchana ambapo walipelekwa polisi na kutoka lakini baadaye waliyamaliza.

Sababu kubwa ya wasanii hao kumvamia mwanadada Hamisa ilidaiwa kuwa alimchukuwa mwanaume wa mmojawapo (Mary) ilihali akijua kwamba ni shemeji yake, jambo ambalo liliwakera na kumuengua kwenye kundi na kuchukua hatua ya kwenda kumvamia.

No comments: