Hans Bonge Music

kwa ajili ya music ungana nami hapa http://www.hulkshare.com/hansbonge

Thursday 5 December 2013

Picha ya kwanza aliyopigwa mpenzi wa mwigizaji Paul Walker toka kifo kitokee.







Girlfriend wa muda mrefu wa mwigizaji Paul Walker aliefariki kwenye ajali ya gari,
ameonekana kwa mara ya kwanza toka kitokee kifo cha mwigizaji huyu aliefariki
November 30 2013 California, U.S.
Girlfriend wake aitwae Jasmine Pilchard-Gosnell alionekana akiwa mnyonge na
anaetokwa machozi mara kwa mara baada ya kuonekana hadharani kwa mara ya
kwanza toka kifo cha Paul kitokee ambapo unazoziona hapo juu ni picha za kwanza
alizopigwa toka kifo cha Paul aliefariki akiwa na umri wa miaka 40 huku girlfriend wake
akiwa na 23.

Saturday 19 October 2013

Jela kweli pamembadilisha LULU, soma hichi alichokisema kuhusu Babu seya na mwanaye

Ninaamini Mungu yupo...anasikia,anaona na ndiye mwenye kuhukumu kwa Haki...!!!!Dua zangu ziko pamoja na Mzee Nguza na Papii Kocha...!hakuna linaloshindikana mbele ya Mwenyezi Mungu...Kama anaweza kutoa Jaribu basi yeye pia ndo mwenye Uwezo wa kufanya Njia ya kutoka ktk jaribu Hilo...!Mwenyezi Mungu awasimamie katika rufaa yenu...!AMEN”
Hayo ni maneno ya mwanadada Elizabeth Michael (LULU) aliyoyaandika kupitia kwenye mtandao akiwaombea kheri Mzee Nguza na mwanawe Papii Kocha wanaosubiria kusikilizwa kwa rufaa yao ya kesi ya ulawiti inayowakabili
Toka atoke jela, mwanadada lulu ameonekana kubadilika sana kitabia tofauti na alivyokuwa akionekana hapo awali.